TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku hui Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Mabao ya Azam FC yamefungwa na kiungo Feisal Salum Abdallah dakika ya tatu na mshambuliaji mpya, Jean-Jacques Ngita Kamanga raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), aliyesajiliwa dirisha dogo kutoka Aris Limassol ya Cyprus mawili dakika ya 19 na 59.
Kwa ushindi huo, Azam FC wanafikisha pointi 22 katika mchezo wa 10 na kupanda kwa nafasi tatu hadi ya tano, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake 21 za mechi 16 nafasi ya nne.

.png)
0 comments:
Post a Comment