• HABARI MPYA

  Friday, December 01, 2023

  TABORA UNITED YAWALAMBA MTIBWA SUGAR 2-1 MWINYI


  WENYEJI, Tabora United wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora.
  Mabao ya Tabora United yamefungwa na Eric Okutu dakika ya 19 na Ben Nakibinge dakika ya 32, wakati bao pekee la Mtibwa Sugar limefungwa na Kassim Haruna dakika ya 75.
  Kwa ushindi huo, Tabora United inafikisha pointi 14 katika mchezo wa 10 na kusogea nafasi ya nane, wakati Mtibwa Sugar wanazidi kukaza msuli ili kuzibeba timu nyingine zote 15 za Ligi Kuu wakiwa wanashika mkia kwa pointi zao tano baada ya kucheza mechi 11.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TABORA UNITED YAWALAMBA MTIBWA SUGAR 2-1 MWINYI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top