MABINGWA watetezi, Yanga SC wamefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa mabao 7-1 dhidi ya Polisi Tanzania usiku huu Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
Mkali wa Yanga leo ni mshambuliaji Muangola, Laurindo Dilson Maria Aurélio ‘Depu’ aliyefunga mabao matatu dakika za 22 34 na 59 baada ya kiungo Mudathir Yahya Abbas kufunga bao la kwanza dakika ya kwanza.
Mabao mengine ya Yanga yamefungwa na beki Joseph Majagi aliyejifunga dakika ya 38, winga Mgambia Buba Jammeh dakika ya 76 na kiungo Abdulnassir Mohamed ‘Casemiro’ dakika ya 84, wakati bao pekee la Polisi alijifunga beki Mghana, Frank Assinki dakika ya 81.



.png)
0 comments:
Post a Comment