TIMU ya Mtibwa Sugar imetupwa nje ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Hatua ya 32 Bora michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya kufungwa 1-0 na Mbuni jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Bao pekee la Mbuni inayoshiriki Ligi ya
ya Championship lililoitupa nje Mtibwa Sugar inayocheza Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara limefungwa na Omary Athumani dakika ya 33.
Mchezo mwingine wa Hatua ya 32 Bora Kombe la CRDB leo, timu nyingine ya Championship, TMA Stars ya Arusha imeitoa Tanzania Prisons ya Ligi Kuu kwa kuichapa 1-0 bao la Ernest Baltazari dakika ya 39 Uwanja wa Halmashauri ya Wilaya Chunya Jijini Mbeya.
Nayo Mbeya City imeitoa Bandari FC kwa kuichapa 3-0 mabao ya Vitalis Mayanga dakika ya 16 na 55 na Riphat Msuya dakika ya 76 Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.




.png)
0 comments:
Post a Comment