• HABARI MPYA

  Wednesday, June 08, 2022

  TEMBO WATAKIWA KUITUMIA ULAYA KUSHINDA KOMBE LA DUNIA


  WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na michezo.Mhe, Mohamed Mchengerwa ameitaka Timu ya soka ya walemavu ya (Tembo Warriors) kutumia mechi za maandalizi na nchi mbalimbali za Ulaya kujinoa ili kushinda kombe  hilo.
  Mhe Mchengerwa ametoa kauli hiyo leo Juni 8, 2022 uwanja wa Benjamini Mkapa wakati akiikabidhi bendera ya Taifa timu hiyo akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi inayokwenda kuanza kucheza mashindano kwenye maandalizi na timu  mbalimbali za Ulaya kwa kuanzia na timu ya Poland ili kuweza kupata uzoefu wa kucheza na nchi za mabara mbalimbali  kabla ya kuanza mashindano haya.
  “Tumeamua kama Serikali kuendelea kuhaakikisha kuwa tunazisaidia timu zinazofanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa ili kuwasaidia kukuza ajira na kuwafanya  waajiriwe  kwenye vilabu  vikubwa  duniani” amefafanua Mhe. Mchengerwa 
  Amesema watanzania wamechoka kuona kuwa nchi inasuasua kwenye michezo na amesisitiza kuwa  wakati huu watanzania wanataka  kombe  la dunia kuja  Tanzania ambapo amesema  hilo litafanikiwa kwa kuweka mbele utaifa na uzalendo wanapokuwa kwenye mashindano haya.
  Ameongeza kuwa jambo kubwa kwa sasa ni kuwa na nidhamu na kuzingatia misingi ambayo wanapewa na  makocha wa timu zao ili waweze  kufika mbali na kuboresha  maisha yao na uchumi wan chi yetu kwa ujumla.
  “Naomba kuwaambia mkifanya vizuri katika mashindano  haya ya maandalizi tu nina uhakika  mtanunuliwa na timu kubwa na mtabaki ulaya, mtabadilisha maisha ya familia zenu na watanzania kwa ujumla” ameongeza Mhe. Mchengerwa
  Wakizungumza kwa nyakati tofauti  viongozi wa timu hiyo  wamemwahidi Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kuwa wanakwenda  kuanza kutema cheche  katika maandalizi ya timu hizo za awali ili kujihakikishia  kutwa kombe hilo.
  Katibu Mkuu. Dkt, Abbasi amesema  Tembo Warriors ndiyo timu ya kwanza nchini kufuzu kuingia kwenye mashindano hayo na kuitaka kuendelea kushikilia heshima  hiyo kwa kuwa timu ya kwanza kurejesha kombe  nyumbani.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TEMBO WATAKIWA KUITUMIA ULAYA KUSHINDA KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top