• HABARI MPYA

  Wednesday, June 15, 2022

  AZAM YAICHAPA MBEYA KWANZA 2-0, YAPANDA TATU BORA


  WENYEJI, Azam FC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya Kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na washambuliaji, mzawa Shaaban Iddi Chilunda dakika ya 45 na ushei Mkongo Idris Ilunga Mbombo dakika ya 82.
  Azam FC inafikisha pointi 40 na kupanda nafasi ya tatu, ikiizidi pointi moja baada ya wote kucheza mechi 27, wakati Mbeya Kwanza inabaki na pointi zake 24 za mechi 27 pia ikiendelea kuzibeba timu nyingine 15 katika Ligi Kuu.
  Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka moja kwa moja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 13 na 14 zitamenyana baina yao katika michezo maalum ya mchujo nyumbani na ugenini.
  Timu itakayoshinda itabaki Ligi Kuu, wakati itakayofungwa itamenyana na JKT Tanzania ya Championship na mshindi ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM YAICHAPA MBEYA KWANZA 2-0, YAPANDA TATU BORA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top