• HABARI MPYA

  Sunday, June 26, 2022

  KICHUYA APIGA HAT TRICK NAMUNGO YAICHAPA MTIBWA 4-2


  KIUNGO mshambuliaji, Shiza Ramadhani Kichuya ameifungia mabao matatu Namungo FC ikitoka nyuma na kuichapa timu yake ya zamani, Mtibwa Sugar 4-2 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
  Kichuya amefunga mabao hayo dakika za 24, 51 na 66 huku bao lingine la Namungo likifungwa na Sixtus Sabilo dakika ya 73, wakati ya Mtibwa yamefungwa na Nzigamasabo Steve kwa penalti dakika ya sita na George Makang’a dakika ya 10.
  Namungo FC inafikisha pointi 40 baada ya ushindi huo na kusogea nafasi ya tano, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake 31 nafasi ya 12 baada ya wote kucheza mechi 29.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KICHUYA APIGA HAT TRICK NAMUNGO YAICHAPA MTIBWA 4-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top