// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KILIMANJARO QUEENS YAICHAPA ZANZIBAR QUEENS 12-0 CHALLENGE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KILIMANJARO QUEENS YAICHAPA ZANZIBAR QUEENS 12-0 CHALLENGE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Tuesday, June 07, 2022

  KILIMANJARO QUEENS YAICHAPA ZANZIBAR QUEENS 12-0 CHALLENGE


  TIMU za taifa za Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya michuano ya CECAFA Challenge baada ya ushindi wa 12-0 dhidi ya Zanzibar, Zanzibar Queens jana Uwanja wa FUFA Technical Centre, Njeru katika mechi ya mwisho za Kundi B. 
  Mabao ya Kilimanjaro Queens yalifungwa na Opa Clement manne, Janeth Pangamwene, Diana Msewa, Enekia Kasonga ‘Lunyamila’, Mwanahamisi Omar ‘Gaucho’ matatu, Protas Mbunda na Ester Mabanza.
  Mechi nyingine ya mwisho ya Kundi B, Ethiopia iliichapa Sudan Kusini 4-0 hapo hapo FTC Njeru.
  Sasa Kilimanjaro Queens itamenyana na Burundi katika Nusu Fainali Alhamisi, wakati Ethiopia itawavaa wenyeji, Uganda, wakati Zanzibar na Sudan Kusini zinaungana na Rwanda na Djibouti za Kundi A kuyaaga mashindano hayo.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KILIMANJARO QUEENS YAICHAPA ZANZIBAR QUEENS 12-0 CHALLENGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top