• HABARI MPYA

    Saturday, June 11, 2022

    OPA CLEMENT AWA MFUNGAJI BORA CECAFA CHALLENGE

    MSHAMBULIAJI wa Tanzania, Opa Clement Sanga ameibuka mfungaji bora wa michuano ya CECAFA Challenge Wanawake iliyofikia tamati leo Jinja nchini Uganda.
    Opa anayechezea klabu ya for Kayseri Kadın FK ya Uturuki amekuwa mfungaji bora kutokana na mabao 
    yake saba aliyefunga kwenye michuano hiyo, timu yake, Kilimanjaro Queens ikimaliza nafasi ya nne.
    Aidha, Kilimanjaro Queens iliyofungwa 2-1 na Ethiopia katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu leo imeshinda Tuzo ya Timu yenye Nidhamu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: OPA CLEMENT AWA MFUNGAJI BORA CECAFA CHALLENGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top