• HABARI MPYA

    Monday, June 20, 2022

    NADO AANZA MAZOEZI MEPESI AZAM AREJEE MSIMU UJAO


    KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC, Idd Suleiman 'Nado' anatarajiwa kurejea uwanjani mwanzoni mwa msimu ujao baada ya kuwa nje tangu Novemba 30 mwaka jana.
    Taarifa ya Azam FC imesema FC Nado aliyeumia dakika ya 29 tu kwenye mechi na Mtibwa Sugar anaendelea vyema baada ya kuanza programu ya mazoezi mapesi kabla ya kurejea dimbani kucheza tena soka la ushindani.
    Daktari Mkuu wa Azam FC, Dk. Mwanandi Mwankemwa, amethibitisha kuwa Nado atarejea dimbani kwa soka la ushindani Septemba mwaka huu.
    Aidha, Mwankemwa amesema Nado ataruhusiwa kuanza mazoezi na wenzake, wakati Azam FC itakapoanza maandalizi rasmi ya kujiandaa na msimu ujao.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NADO AANZA MAZOEZI MEPESI AZAM AREJEE MSIMU UJAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top