• HABARI MPYA

  Wednesday, June 15, 2022

  MAYELE APIGA MBILI, YANGA BINGWA LIGI KUU


  VIGOGO, Yanga SC wamejihakikishia ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanya usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Yanga leo yamefungwa na washambuliaji wake Wakongo, Fiston Kalala Mayele, mawili dakika ya 35 na 68 na Chico Ushindi Wakubanza dakika ya 52.
  Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 67 katika mchezo wa 27, ambazo hakuna inayoweza kufikisha, kwani mabingwa wa misimu minne iliyopita wenye pointi 51 sasa wanaweza kufikisha pointi 66 kama watashinda mechi zao zote tano zilizosalia.
  Coastal Union inabaki na pointi zake 34 za mechi 37 sasa na kushuka kwa nafasi moja hadi ya saba.
  Coastal Union na Yanga watakutana tena katika Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) Julai 2 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYELE APIGA MBILI, YANGA BINGWA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top