// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MPOLE AMFIKIA MAYELE GEITA GOLD YAICHAPA BIASHARA 2-0 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MPOLE AMFIKIA MAYELE GEITA GOLD YAICHAPA BIASHARA 2-0 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Saturday, June 18, 2022

  MPOLE AMFIKIA MAYELE GEITA GOLD YAICHAPA BIASHARA 2-0


  WENYEJI, Geita Gold wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Biashara United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita.
  Mabao ya Geita Gold yamefungwa na washambuliaji wake tegemeo, George Mpole dakika ya 29 na Edmund John dakika ya 66 na kwa ushindi huo, Geita Gold inafikisha pointi 42 katika mchezo wa 28 na kupanda nafasi ya tatu, ikiizidi pointi mbili Azam FC, ambayo hata hivyo ina mechi moja mkononi.
  Aidha, Mpole leo amefikisha mabao 16 akimfikia mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele wa mabingwa tayari, Yanga wawili hao wakiendelea kuchuana jino kwa jino kuwania ufungaji Bora wa Ligi Kuu.
  Mambo yanazidi kuwa magumu kwa Biashara United ikibaki na pointi zake 25 nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16 kueleka mechi mbili za mwisho.
  Ikumbukwe timu mbili za mwisho zitateremka moja kwa moja na zitakazomaliza nafasi ya 13 na 14 zitamenyana baina yao katika mechi mbili maalum za nyumbani na ugenini, itakayoshinda ndiyo inabaki Ligi Kuu.
  Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na JKT Tanzania kutoka Championship katika mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi ndiye atacheza tena Ligi Kuu msimu ujao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MPOLE AMFIKIA MAYELE GEITA GOLD YAICHAPA BIASHARA 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top