• HABARI MPYA

    Monday, June 13, 2022

    GEITA GOLD 2-0 DODOMA JIJI, MTIBWA 3-1 RUVU


    WENYEJI, Geita Gold wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita.
    Mabao ya Geita Gold yamefungwa na Edmund John dakika ya 45 na George Mpole dakika ya 78 na kwa ushindi huo, wanafikisha pointi 39 katika mchezo wa 27 na kupanda nafasi ya tatu, ikiizidi pointi mbili Namungo FC ambayo hata hivyo ina mechi moja mkononi.
    Dodoma Jiji baada ya kichapo cha leo katika mchezo wa 27 inabaki na pointi zake 31 na kushuka kwa nafasi moja hadi ya 12.   
    Katika mchezo uliotangulia mchana wa leo, wenyeji wengine, Mtibwa Sugar waliichapa Ruvu Shooting mabao 3-1 Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
    Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Ally Kombo aliyejifunga dakika ya 41 na Brian Mayanja mawili, dakika ya 56 na 76, wakati la Ruvu Shooting limefungwa na Abal Kassim dakika ya 86.
    Mtibwa Sugar inafikisha pointi 31 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 11, wakati Ruvu Shooting inabaki na pointi zake  28 katika nafasi ya 13 baada ya timu zote kucheza mechi 27 sasa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GEITA GOLD 2-0 DODOMA JIJI, MTIBWA 3-1 RUVU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top