• HABARI MPYA

  Tuesday, June 14, 2022

  KMC YATOA SARE NA PRISONS 1-1 DAR


  WENYEJI, KMC wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  KMC walitangulia na bao la Matheo Anthony dakika ya pili tu kabla ya Jeremiah Juma kuisawazishia Prisons dakika ya 16.
  KMC inafikisha pointi 32 katika mchezo wa 26, ingawa inabaki nafasi ya 10 na Prisons inatimiza pointi 26 katika mchezo wa 27 na inabaki nafasi ya 14 katika Ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili zitashuka.
  Timu zitakazomaliza nafasi ya 13 na 14 zitamenyana baina yao katika michezo maalum ya mchujo nyumbani na ugenini na itakayoshinda itabaki Ligi Kuu, wakati itakayofungwa itamenyana na JKT Tanzania ya Championship na mshindi ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KMC YATOA SARE NA PRISONS 1-1 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top