// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA YA MATOLA YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA YA MATOLA YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Thursday, June 23, 2022

  SIMBA YA MATOLA YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI


  VIGOGO, Simba SC wamewaaga mashabiki wao kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara wa mwisho nyumbani msimu huu.
  Nyota kutoka Senegal, Pape Ousmane Sakho alianza kuifungia Simba dakika ya 16 akimalizia pasi ya Kibu Dennis, kabla ya kumsetia kiungo mwenzake, Mmalawi, Peter Banda kufunga bao la pili dakika ya 43.
  Huo ni mchezo wa tatu mfululizo Simba inashinda chini ya kocha wa muda Suleiman Matola baada ya kufukuzwa Mspaniola, Pablo Franco Martin, ikitoka kushinda 3-1 dhidi ya 3-0 dhidi ya Mbeya City na 3-1 dhidi ya KMC, zote Uwanja wa Mkapa.
  Kwa ushindi huo, Simba inafikisha pointi 60, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi 10 na mabingwa tayari, Yanga SC baada ya wote kucheza mechi 28 kuelekea mechi mbili kukamilisha msimu.
  Mtibwa Sugar wenyewe baada ya kuchapwa leo wanabaki na pointi zao 31 za mechi 28 pia nafasi ya 12 katika Ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili zitateremka daraja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YA MATOLA YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top