// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); WAZIRI MKUU MGENI RASMI TAMASHA LA UTAMADUNI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE WAZIRI MKUU MGENI RASMI TAMASHA LA UTAMADUNI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, June 28, 2022

    WAZIRI MKUU MGENI RASMI TAMASHA LA UTAMADUNI


    WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi kwenye Tamasha la kwanza la kihistoria la Utamaduni  kitaifa  Julai 2, 2022  Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
    Tamasha hilo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania aliyoyatoa kwenye Tamasha la Utamaduni la Mkoa wa Kilimanjaro la kutaka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuandaa tamasha kubwa la kitaifa la utamaduni litakaloshirikisha mikoa yote ya Tanzania ili kutangaza hazina ya utamaduni wa makabila ya Tanzania Duniani.
    Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amefafanua kuwa tamasha hilo litaambatana na matembezi maalum ya kitamaduni (Utamaduni Carnival) katika jiji la Dar es Salaam ambayo yameandaliwa njia  maalum za kupita ikiwemo daraja la juu la Mfugale, Kijazi, Tanzanite na daraja la mwalimu Nyerere.
    Amesema,  tamasha hilo litatoa fursa kwa  makabila yote  nchini kuonesha  tamaduni zao kupitia  ngoma na vyakula vya asili  ili kukuza utalii wa kiutamaduni.
    Aidha, amewataka watanzania  kujitokeza kushiriki kwenye  tamasha hilo la kwanza la kitaifa ambalo licha ya kutoa  burudani,  litaonesha  vitu  muhimu vya kiutamaduni na kutoa fursa kwa wageni kujifunza.
    Ameongeza  kuwa, tamasha hilo litakuwa  la siku tatu ambapo siku  inayofuata ya Julai 3, 2022  itakuwa  na tukio maalum la  mirindimo  ya taarabu ambapo limeainishwa kama usiku wa taarabu utakaofanyika eneo la  ufukwe wa Coco Beach  maarufu kwa wachoma mihogo kuanzia saa 8:00 hadi saa 6:00 usiku.
    Amesema shamrashamra hizo zitashamirishwa na vikundi mbalimbali vya wasanii kutoka ndani na nje ya Tanzania kama Comoro, Burundi na Kenya,  pia wasanii  wa taarabu nchini akiwemo  Mzee Yusufu, Hadija Kopa, Patricia Hillay, Abuduli Misambano na Aisha Mashauzi watakuwepo kutumbuiza usiku huo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAZIRI MKUU MGENI RASMI TAMASHA LA UTAMADUNI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top