• HABARI MPYA

  Monday, June 20, 2022

  SAMATTA AREJEA FENERBAHCE BAADA YA KUMALIZA MKOPO ANTWERP


  MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amerejea klabu yake, Fenerbahçe ya Uturuki baada ya kuwa kwa mkopo Royal Antwerp ya Ubelgiji msimu wote uliopita.
  Samatta alitua kwa mkopo Fenerbahçe Septemba 25 mwaka 2020 kutoka Aston Villa ya England ambako alisajiliwa kwa mkataba wa miaka minne na nusu Januari 20 mwaka 2020 kutoka KRC Genk ya Ubelgiji.
  Baada ya kufunga mabao matano katika mechi 27 akanunuliwa moja kwa moja Fenerbahçe akisaini mkataba wa miaka minne Julai 2021, lakini Septemba 1 2021 akatolewa kwa mkopo wa muda mrefu Royal Antwerp ambako amecheza mechi 32 na kufunga mabao matano.
  Samatta aliibukia African Lyon mwaka 2008, kabla ya kwenda Simba mwaka 2010, zote za Dar es Salaam, baadaye TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mwaka 2011 kabla ya kununuliwa na Genk mwaka 2016.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AREJEA FENERBAHCE BAADA YA KUMALIZA MKOPO ANTWERP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top