• HABARI MPYA

    Thursday, June 16, 2022

    YANGA YASAJILI MSHAMBULIAJI WA CHIPOLOPOLO NA KAIZER


    MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga SC wamemtambulisha mshambuliaji wa Kimataifa wa Zambia, Lazarous Kambole kuwa mchezaji wake mpya wa kwanza kuelekea msimu ujao.
    Kambole mwenye umri wa miaka 28, anatua Jangwani akitokea Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini aliyojiunga nayo mwaka 2019 akitokea ZESCO United ya kwao.
    Kambole aliibukia Konkola Mine Police mwaka 2011, kabla ya kuhamia Konkola Blades mwaka 2013 ambako alicheza hadi 2014 alipokwenda ZESCO United - na tangu mwaka 2018 amekuwa akichezea timu ya taifa, Chipolopolo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA YASAJILI MSHAMBULIAJI WA CHIPOLOPOLO NA KAIZER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top