// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NDONDO CUP KURUSHWA LIVE TV 3 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NDONDO CUP KURUSHWA LIVE TV 3 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Thursday, June 02, 2022

  NDONDO CUP KURUSHWA LIVE TV 3


  KITUO cha Television cha  TV3 kilichopo kwenye King'amuzi cha Star TV, kitaonyesha Moja kwa Moja mashindano ya Ndondo Cup yanayotarajia kuanza kutimua vumbi Julai 3 mwaka huu.   
  Akizungumza na waandishi wa Habari Mkurugenzi wa Tv3 Ramadhan Msemo, alisema kuwa Tv3 wameona sehemu sahihi na kupata haki na nafasi ya kutoa nafasi kuonekana kuanzia ufunguzi hadi Fainali.              
  Alisema Ndondo cup ni sehemu ya kuwalea watu kimichezo na kuona vipaji tofauti vya vijana ambao walikuwa mtaani, walikuwa hawajui watapata lini nafasi ya kucheza na kuonekana.
  "Ukiiwa na maarifa basi una uwezo wa kutosha, inagusa Kila sekta ya Afya, michezo, biashara".                 
  "Katika mashindano haya timu ya Mshikamano city ina kocha mwanamke ni Jambo kubwa Sana, yote yametokana na michuano hii ya Ndondo Cup"Alisema.
   wa michuano hiyo Yahya Mohamed, alisema michuano hiyo ina Imefikisha miaka 9 tangu ianzishwe.
  Alisema kutokana na majadiliano wazo lilianzia pale na kuona Kuna haja ya kuanzisha michuano ya ndondocup au Mashindano ya mtaani 
  Alisema mfumo wa uendeshaji was kombe la Dunia Kwa Timu 32 kisajili na mchezo wa ufunguzi ulifanyika shule ya makurumla.
  Aliizitaja faida za kuwapa nafasi vijana kuonekana na manufaa ikiwemo kelvin sabato maarufu kama "Kiduku, idi Suleiman Nado ,golikipa Mandanda 
  "Kuwasaidia wachezaji kupata nafasi na kadri muda ulivokua ukisonga makocha walikua wakihitaji Mabadiliko,
  .Timu jaribu zote zinazoshirki ndondo cup wasomi na Wana vyeti na kutambulika .
  Alisema kuwa kupitia mashindano hayo  wametengeneza makocha na waamuzi ambao wanajiendeleza na wengine kukuwa zaidi.
  "Kuna waamuzi kama Ramadhan Kayoko,Heri Sasi ni Misingi bora ya  michuano ya  ndondocup tumekuwa daraja la kusaidia, walikuwa hawana nafasi, kupata nafasi"alisema Mohammed.
  Alisema katika michuano huo jumla ya timu 72, zitapambana kupata Bingwa wa michuano hiyo.
   
  Mdhamini Mwenza Issa Masoud, alisema kuwa  kwa kushirikiana na uongozi wa Startimes zawadi Kwa bingwa milioni 20 na mahindi pili atapata sh.milioni 10.
  Masoud alisema kuwa  timu zilizoingia hatua zitapewa million 2 na kikundi Bora Cha uhamasisha million 1.
  Masoud alisema timu zinatoka mtaani hazina Hali nzuri hivyo tumeruhusu watafute wadhamini wao kukaa kwenye jezi Ili waweze kupata kipato waweze kujiendesha.
  Aidha Masoud alisema Mikoa itakayoweza kushiriki Dodoma, Mwanza, Shinyanga, Njombe, Mtwara imesibitisha ushiriki
  Kupitia michuano hiyo kuna fursa kwa Wafanyabiashara wadogo wadogo kufanya biashara kutokana na mkusanyiko wa watu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NDONDO CUP KURUSHWA LIVE TV 3 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top