• HABARI MPYA

  Wednesday, June 22, 2022

  YANGA YAICHAPA POLISI 2-0 NA KUZIDI KUUSTAWISHA UBINGWA


  VIGOGO, Yanga SC wamezidi kuustawisha ubingwa wao baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Yanga yamefungwa na Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ dakika ya 12 na Chico Ushindi Wakubanza dakika ya 17 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 70 katika mchezo wa 28, sasa wakiwazidi pointi 13 washindi wa pili tayari, Simba SC ambao wamecheza mechi 28.
  Polisi Tanzania inabaki na pointi zake 36 za mechi 28 sasa nafasi ya saba.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, wenyeji KMC wameitandika Mbeya Kwanza mabao 4-1 Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAICHAPA POLISI 2-0 NA KUZIDI KUUSTAWISHA UBINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top