• HABARI MPYA

  Monday, June 06, 2022

  SERENGETI GIRLS YAFUZU KOMBE LA DUNIA U17



  TIMU ya Taifa ya wasichana chini ya umri wa miak 17, Serengeti Girls imefanikiwa kufuzu Fainali za Kombe la Dunia baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Cameroon Jumapili Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Katika mchezo huo wa marudiano Raundi ya mwisho ya mchujo kuwania tiketi ya Fainali zitakazofanyika Oktoba nchini India, bao pekee la Tanzania lilifungwa na Neema Paul Kinega.
  Serengeti Girls inafuzu Fainali za kwanza za Kombe la Dunia kwa ushindi wa jumla wa 5-1 kufuatia kushinda 4-1 kwenye mechi ya kwanza Yaoundé.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERENGETI GIRLS YAFUZU KOMBE LA DUNIA U17 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top