TANZANIA imepangwa Kundi D pamoja na Canada, Japan na Ufaransa katika Fainali za Kombe la Dunia la Wanawake chini ya umri wa miaka 17 zinazotarajiwa kuanza Oktoba 11 hadi 30, mwaka huu nchini India.
Wenyeji, India wamewekwa Kundi A kama ilivyo ada pamoja na Marekani, Morocco na Brazil, wakati Kundi B linaundwa na Ujerumani, Nigeria, Chile na New Zealand.
Mabingwa watetezi, Hispania walioshinda taji lao la kwanza mwaka 2018 nchini Uruguay wamepangwa Kundi C pamoja na Colombia, Mexico na China.
Serengeti Girls ilifuzu baada ya kuitoa Cameroon kwa jumla ya mabao 5-1, ikishinda 4-1 Jijini Yaoundé, kabla ya kushinda 1-0 Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment