• HABARI MPYA

  Monday, June 13, 2022

  FARID MUSSA AONGEZA MKATABA YANGA HADI 2024


  KIUNGO Farid Mussa Malik ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuchezea Yanga hadi mwaka 2024.
  Farid alijiunga na Yanga mwaka 2020 akitokea Tenerife ya Hispania ambayo alijiunga nayo mwaka 2016 akitokea Azam FC ya nyumbani, Dar es Salaam.
  Ni kipaji ambacho kiliibuliwa katika akademi ya Azam FC, kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa mwaka 2013 ambako alicheza hadi anakwenda Hispania mwaka 2016.
  Pamoja na kusajiliwa Yanga kama kiungo wa pembeni, lakini msimu huu kocha Mtunisia, Nasredine Mohamed Nabi amekuwa akimtumia kama beki wa kushoto pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FARID MUSSA AONGEZA MKATABA YANGA HADI 2024 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top