• HABARI MPYA

  Sunday, June 26, 2022

  TANZANIA PRISONS YAICHAPA SIMBA 1-0 SOKOINE


  WENYEJI, Tanzania Prisons wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya vigogo, Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Bao pekee la Tanzania Prisons limefungwa na Nahodha wake, Benjamin Asukile dakika ya 54 na kwa ushindi huo, wanafikisha pointi 29 za mechi 29 na kusogea nafasi ya 14.
  Kwa upande wao, Simba wanabaki na pointi zake 60 nafasi ya pili nyuma ya mabingwa tayari, Yanga wenye pointi 71 baada ya wote kucheza mechi 29.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA PRISONS YAICHAPA SIMBA 1-0 SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top