• HABARI MPYA

  Thursday, June 16, 2022

  SAKHO APIGA MBILI, SIMBA YAICHAPA MBEYA CITY 3-0


  WENYEJI, Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba yamefungwa na viungo, Msenegal Pape Ousmane Sakho mawili, dakika ya 39 kwa penalti na 55 na Mmalawi, Peter Banda dakika ya 76.
  Simba SC inafikisha pointi 54 katika mchezo wa 26, ingawa inabaki nafasi ya pili nyuma ya mabingwa tayari, Yanga SC wenye pointi 67 za mechi 27, wakati Mbeya City inabaki na pointi zake 32 za mechi 27 pia nafasi ya 10.
  Mechi iliyotangulia, Polisi Tanzania imewachapa wenyeji, Namungo FC 2-1 Uwanja wa Ilulu mjini Lindi.
  Bao la Namungo Hussein Bakari wa alijifunga dakika ya pili, kabla ya Tariq Seif kuisawazishia Polisi Tanzania dakika ya 45 na kufunga la ushindi dakika ya 70.
  Polisi inafikisha pointi 36 na kusogea nafasi ya sita, huku Namungo ikibaki na pointi zake 37 katika nafasi ya tano baada ya wote kucheza mechi 27.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAKHO APIGA MBILI, SIMBA YAICHAPA MBEYA CITY 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top