• HABARI MPYA

  Thursday, June 30, 2022

  MRENO NDIYE KOCHA MPYA AL AHLY


  KLABU ya Al Ahly ya Misri imemtambulisha Mreno, 
  José Ricardo Soares Ribeiro kuwa kocha wake mpya Mkuu akichukua nafasi ya Muafrika Kusini, Pitso Mosimane aliyefukuzwa mwezi huu.
  Soares, ambaye ni winga wa zamani wa Kimataifa wa Ureno, anajiunga na mabingwa hao wa kihistoria Afrika akitokea klabu ya Gil Vicente FC ya kwao, Ureno.
  Mosimane aliondolewa kazini baada ya Ahly kufungwa na Wydad Casablanca katika Fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MRENO NDIYE KOCHA MPYA AL AHLY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top