• HABARI MPYA

  Friday, June 17, 2022

  SIMBA YATHIBITISHA KUMUUZA BWALYA AFRIKA KUSINI


  KLABU ya Simba SC imethibitisha kumuuza kiungo wake Mzambia, Rally Bwalya ambaye anakwenda kujiunga na Amazulu ya Afrika Kusini kwa mkataba wa mkataba wa miaka wa miwili.
  Bwalya, ambaye kwao Zambia anajulikana kwa jina la utani, Kamuchacha au Soft Touch, alijiunga na Simba Agosti mwaka 2020 akitokea Power Dynamos ya kwao, Lusaka kwa mkataba wa miaka mitatu ambao ulitarajiwa kumalizika mwakani.
  Katika kipindi cha misimu miwili ya kuwa na Wekundu wa Msimbazi ameiwezesha timu kushinda mataji matatu msimu uliopita, Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) na kufika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Msimu huu ameshinda Kombe la Mapinduzi na kuifikisha Simba Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YATHIBITISHA KUMUUZA BWALYA AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top