• HABARI MPYA

  Tuesday, June 28, 2022

  KOCHA MSAUZI WA MAKIPA SIMBA ATIMKIA ORLANDO

  KOCHA wa makipa wa klabu ya Simba SC, Tyron Damons ameagwa rasmi na imeelezwa anakwenda kujiunga na klabu ya Orlando Pirates ya kwao, Afrika Kusini.
  “Klabu ya Simba inamtakia kila la heri Kocha wa magoli kuondoka klabuni kwetu mwishoni mwa msimu huu,”
  “Tyron amepata kazi kunako klabu ya Orlando Pirates ya nchini kwao Afrika Kusini na tayari amewasilisha ombi la kutaka kuondoka klabuni kwetu na kujiunga na miamba hiyo ya Afrika Kusini,” imesema taarifa ya Simba SC.
  Aidha, taarifa hiyo imeongeza kwamba tayari mchakato wa kutafuta mrithi wa Tyron umeanza na dhamira ni kumpata kocha mpya wa makipa kabla ya kuanza kwa maandalizi ya msimu mpya. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOCHA MSAUZI WA MAKIPA SIMBA ATIMKIA ORLANDO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top