• HABARI MPYA

  Tuesday, June 21, 2022

  SIMBA SC YAAGANA NA WAWA BAADA YA MIAKA MITANO


  KLABU ya Simba imetangaza kuachana na beki wake, Serges Pascal Wawa Sfondo baada ya msimu huu, kufuatia Muivory Coast huyo kuwatumia Wekundu wa Msimbazi tangu mwaka 2017.
  Wawa mwenye umri wa miaka 36 sasa, mzaliwa wa Bingerville, Ivory Coast alitua Simba akitokea El-Merreikh ya Sudan ambako alikuwa anacheza kwa mara ya pili.
  Haswa kisoka aliibukia ASEC Mimosas mwaka 2003 ambako alicheza hadi 2010 alipokwenda El-Merreikh alikocheza hadi 2014 akahamia Azam FC ya Dar es Salaam.
  Mwaka 2016 alirejea Al-Merrikh kwa msimun mmoja, kabla ya kurejea Tanzania na kujiunga na Simba SC.
  Katika kipindi hicho cha miaka mitano, Wawa ameshinda mataji manne ya Ligi Kuu akiwa na Simba,   2017–18, 2018–19, 2019–20 na 2020–21, Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) mawili, 2019–20 na 2020–2021, Ngao za Jamii nne 2017, 2018, 2019 na 2020 na Kombe la Mapinduzi mara tatu, 2011, 2015 na 2022.
  Lakini pia amewezesha Simba kufika Robo Fainali ya Ligi Mabingwa mara mbili, 2018–19 na 2020–21 pamoja na Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAAGANA NA WAWA BAADA YA MIAKA MITANO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top