// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AUSTRALIA YAFUZU KOMBE LA DUNIA MARA YA TANO MFULULIZO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AUSTRALIA YAFUZU KOMBE LA DUNIA MARA YA TANO MFULULIZO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Tuesday, June 14, 2022

  AUSTRALIA YAFUZU KOMBE LA DUNIA MARA YA TANO MFULULIZO


  SHANGWE nzito zilitawala jana Uwanja wa Ahmad Bin Ali Jijini Al Rayyan kufuatia Australia kuwa timu ya 31 kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar kwa ushindi wa mikwaju ya penalti dhidi ya Peru (Amerika Kusini) kwenye mchezo wa mchujo wa intercontinental.
  Kipa Andrew Redmayne, aliyechukua nafasi ya Mathew Ryan kabla ya kuanza matuta ndiye aliibuka shujaa baada ya kuokoa penalty ya mwisho ya Alex Valera.
  Hii inakuwa mara ya tano mfululizo Australia kufuzu Kombe la Dunia tangu mwaka 2006 na sasa wataingia Kundi D pamoja na mabingwa watetezi, Ufaransa, Denmark na Tunisia.
  Timu ya 32 na ya mwisho kuingia kwenye fainali za Qatar itapatikana leo katika Uwanja huo huo, wakati wawakilishi wa CONCACAF, Costa Rica watakapomenyana na wawakilishi OFC, New Zealand katika intercontinental play-off nyingine.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AUSTRALIA YAFUZU KOMBE LA DUNIA MARA YA TANO MFULULIZO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top