• HABARI MPYA

  Thursday, June 30, 2022

  YUSSUF BAKHRESA AMEAMUA, ASHUSHA MUIVORY COAST MWINGINE AZAM


  KLABU ya Azam FC imetambulisha mchezaji mwingine kutoka Ivory Coast, naye pia kiungo mshambuliaji, Tape Edinho aliyesaini mkataba wa miaka mitatu.
  Azam FC imemnunua Edinho tumemnunua kutoka ES Bafing ya kwao, ambapo mkataba huo utamfanya kuhudumu ndani ya viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2025.
  Usajili wa nyota huyo mwenye uwezo mkubwa umekamilishwa na Mkurugenzi timu, Yusuf Bakhresa akishirikiana na Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat'.
  Mkali huyo amechaguliwa kwenye kikosi bora cha Ligi Kuu ya Ivory Coast (Ligue 1) msimu huu, kutokana na ubora wake wa kuhenyesha wachezaji wa timu pinzani.
  Msimu uliomalizika, amefanikiwa kufunga jumla ya mabao matano na kuchangia pasi tisa zilizozaa mabao.
  Anakuwa Muivory Coast wa pili kutambulishwa leo baada ya 
  Kipre Junior Zunon kutokea Sol FC ya kwao pia ambaye naye amesaini mkataba wa miaka mitatu.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YUSSUF BAKHRESA AMEAMUA, ASHUSHA MUIVORY COAST MWINGINE AZAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top