• HABARI MPYA

  Friday, April 30, 2021

  SIMBA SC KUMENYANA NA KAIZER CHIEFS YA AFRIKA KUSINI ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA MEI 15

   TIMU ya Simba SC ya Tanzania itakutana na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini katika Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya droo iliyopangwa leo Jijini Cairo nchini Misri.
  Mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri nao watamenyana na wapinzani kutoka Afrika Kusini, Mamelodi Sundowns. 
  Mshambuliaji Mtanzania, Simon Happygod Msuva yeye timu yake, Wydad Casablanca itamenyana na MC Alger ya Algeria. CR Belouizdad ya Algeria pia yenyewe itamenyana na vigogo wengine wa Afrika, Esperance ya Tunisia.
  Mechi za kwanza zitachezwa kati ya Mei 14 na 15 na marudiano ni Mei 21 na 22, Simba SC wakianzia nyumbani Dar es Salaam.


  ROBO FAINALI
  Al Ahly vs Mamelodi Sundowns. 
  MC Alger vs Wydad Casablanca. 
  CR Belouizdad vs Esperance. 
  Kaizer Chiefs vs Simba SC. 
  NUSU FAINALI 
  MC Alger / Wydad Casablanca VS  Kaizer Chiefs / Simba SC. 
  CR Belouizdad / Esperance VS Al Ahly / Mamelod Sundowns.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC KUMENYANA NA KAIZER CHIEFS YA AFRIKA KUSINI ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA MEI 15 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top