• HABARI MPYA

  Sunday, April 18, 2021

  MANCHESTER UNITED YAITANDIKA BURNLEY 3-1 OLD TRAFFORD

   

  TIMU ya Manchester United imeichapa Burnley mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuubya England leo Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Mabao ya Man United yamefungwa na Mason Greenwood dakika ya 48 na 84 na Edinson Cavani dakika ya 90 na ushei, wakati la Burnley limefungwa na James Tarkowski dakika ya 50.
  Kwa ushindi huo, Man United imefikisha pointi 66 na sasa inazidiwa pointi nane na mahasimu wao wa Jiji, Manchester City baada ya wote kucheza mechi 32.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANCHESTER UNITED YAITANDIKA BURNLEY 3-1 OLD TRAFFORD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top