• HABARI MPYA

  Thursday, April 29, 2021

  NAMUNGO FC YAKAMILISHA MECHI ZAKE ZA KUNDI D KUCHAPWA 1-0 NA PYRAMIDS FC CAIRO

   TIMU ya Namungo FC imekamilisha mechi zake za Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuchapwa 1-0 na wenyeji, Pyramids FC usiku wa Jumatano Uwanja wa Jeshi la Anga wa Juni 30 Jijini Cairo, Cairo.
  Bao pekee la Pyramids limefungwa na kiungo Mmisri, Ibrahim Adel dakika ya 65.
  Kwa matokeo hayo Pyramids inafikisha pointi 12 na kumaliza nafasi ya pili, nyuma ya Raja Casablanca yenye pointi 15 ambayo itakamilisha mechi zake kwa kumenyana na Nkana FC yenye pointi sita Jijini Casablanca nchini Morocco.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAMUNGO FC YAKAMILISHA MECHI ZAKE ZA KUNDI D KUCHAPWA 1-0 NA PYRAMIDS FC CAIRO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top