• HABARI MPYA

  Saturday, April 17, 2021

  YANGA SC YAZINDUKA NA KUICHAPA BIASHARA UNITED 1-0 BAO PEKEE LA YACOUBA SOGNE DAR

   

  YANGA SC wamezinduka na kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Biashara United ya Mara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee Mburkinabe. Yacouba Sogne dakika ya 58 akimalizia kwa kichwa krosi ya beki wa kushoto, Adeyoum Saleh, huo ukiwa ushindi wa kwanza kwa Yanga ndani ya mechi nne.
  Ushindi huo unaifanya Yanga SC ifikishe pointi 54 baada ya kucheza mechi 24 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi nne zaidi ya Azam FC ambayo hata hivyo imecheza mechi moja zaidi.
  Mabingwa watetezi, Simba SC ambao watamenyana na Mwadui FC mjini Shinyanga wanaendelea kushika nafasi ya tatu kwa pointi zao 49 za mechi 21.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAZINDUKA NA KUICHAPA BIASHARA UNITED 1-0 BAO PEKEE LA YACOUBA SOGNE DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top