• HABARI MPYA

  Sunday, April 04, 2021

  JOTA APIGA MBILI SALAH MOJA LIVERPOOL YAITANDIKA ARSENAL 3-0 EMIRATES


  MABINGWA waliopoteza matumaini ya kutetea taji, Liverpool wameibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya wenyeji, Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa Emirates, London.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na Diogo Jota dakika ya 64 na 82 na Mohamed Salah dakika ya 68 na kwa ushindi huo timu ya Jugern Klopp inafikisha pointi 49 baada ya kucheza mechi 30 na kusogea nafasi ya tano, ikizidiwa pointi 25 na vinara, Manchester City, wakati Arsenal inabaki na pointi zake 42 za mechi 30 sasa katika nafasi ya tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JOTA APIGA MBILI SALAH MOJA LIVERPOOL YAITANDIKA ARSENAL 3-0 EMIRATES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top