• HABARI MPYA

  Sunday, April 25, 2021

  PRINCE DUBE AWAMALIZA YANGA DAKIKA ZA LALA SALAMA, AIFUNGIA BAO PEKEE AZAM FC YASHINDA 1-0 DAR

   

  BAO pekee la mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo dakika ya 86 limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya vigogo, Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Kwa ushindi huo, Azam Fc imefikisha pointi 54 baada ya kucheza mechi 28, ingawa inabaki ya tatu ikizidiwa pointi tatu na Yanga ambayo pia ina mechi moja mkononi.
  Mabingwa watetezi, Simba wanaendelea kutawala kileleni kwa pointi zao 58 za mechi 24.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PRINCE DUBE AWAMALIZA YANGA DAKIKA ZA LALA SALAMA, AIFUNGIA BAO PEKEE AZAM FC YASHINDA 1-0 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top