• HABARI MPYA

  Friday, April 16, 2021

  ARSENAL YAUA 4-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI EUROPA LEAGUE

   

  TIMU ya Arsenal imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya UEFA Europa League baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya wenyeji, Slavia Praha usiku huu Uwanja wa Sinobo Stadium Jijini Praha.
  Mabao ya Arsenal yamefungwa na Nicolas Pépé dakika ya 18, Alexandre Lacazette mawili, moja kwa penalti dakika ya 77 akimalizia pasi ya mfungaji wa bao la kwanza na Bukayo Saka dakika ya 24.
  Arsenal inasonga mbele kwa ushindi wa 5-1 baada ya sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza na itakutana na Villarreal iliyoitoa Dinamo Zagreb.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAUA 4-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top