• HABARI MPYA

  Monday, April 19, 2021

  KOCHA JOSE MOURINHO ATUPIWA VIRAGO TOTTENHAM HOTSPUR


  KLABU ya Tottenham imemfukuza Mreno Jose Mourinho kutokana na mwenendo mbaya wa timu kwenye Ligi Kuu ya England na sasa kocha wa 
  RB Leipzig, Julian Nagelsmann anatajwa kuchukua nafasi yake. 
  Mourinho, mwenye umri wa miaka 58, alichukua nafasi ya Mauricio Pochettino aliyefukuzwa Novemba 2019, lakini naye amefukuzwa kufuatia  matokeo mabaya kwenye michuano ya nyumbani na Europa League.
  Na hatua hiyo inakuja ndani ya wiki moja kabla ya Tottenham kumenyana na Manchester City katika fainali ya Carabao Cup Uwanja wa Wembley Aprili 25.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOCHA JOSE MOURINHO ATUPIWA VIRAGO TOTTENHAM HOTSPUR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top