• HABARI MPYA

  Friday, April 09, 2021

  AZAM FC YAREJEA NAFASI YA PILI LIGI KUU BAADA YA KUICHAPA MTIBWA SUGAR 2-0 MABAO YOTE KAFUNGA PRINCE DUBE


  AZAM FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Pongezi kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe, Prince Dube Mpumelelo aliyefunga mabao yote hayo, la kwanza kwa penalti dakika ya tisa na lingine dakika ya 87 akimalizia pasi ya kiungo Mzanzibari, Mudathir Yahya Abbas.
  Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 47 baada ya mechi 25 na kupanda nafasi ya pili ikizidiwa pointi tatu na vigogo, Yanga SC ambao hata hivyo wana mechi mbili mkononi.
  Mabingwa watetezi, Simba SC ni wa tatu wakiwa na pointi 46 za mechi 20.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAREJEA NAFASI YA PILI LIGI KUU BAADA YA KUICHAPA MTIBWA SUGAR 2-0 MABAO YOTE KAFUNGA PRINCE DUBE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top