• HABARI MPYA

  Wednesday, April 14, 2021

  PSG WAIVUA UBINGWA WA ULAYA BAYERN, WATINGA NUSU FAINALI

  TIMU ya Paris Saint-Germain imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya kuchapwa 1-0 na mabingwa watetezi, Bayern Munich katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali Uwanja wa Parc des Princes Jijini Paris.
  Bao pekee la Bayern Munich limefungwa na nyota wa zamani wa PSG, Jean-Eric Maxim
  Last Choupo-Moting dakika ya 40.
  PSG inasonga mbele kwa faida ya mabao ya ugenini, baada ya sare ya jumla ya 3-3 kufuatia kushinda 3-2 kwenye mchezo wa kwanza Munich wiki iliyopita.

  Matokeo hayo ni sawa na PSG kulipa kisasi baada ya kufungwa na Bayern Munich kwenye Fainali ya michuano hiyo msimu uliopita Agosti 23 mwaka jana nchini Ureno.
  Sasa PSG itakutana na mshindi wa jumla kati ya Manchester City na Borussia Dortmund zinazorudiana kesho Uwanja wa Signal-Iduna-Park Jijini Dortmund baada ya timu ya Ujerumani kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza England.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PSG WAIVUA UBINGWA WA ULAYA BAYERN, WATINGA NUSU FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top