• HABARI MPYA

  Saturday, April 03, 2021

  WEST BROM YAICHAPA CHELSEA 5-2 PALE PALE DARAJANI


  TIMU ya West Bromwich Albion leo imeichapa Chelsea 5-2 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London, hicho kikiwa kipigo cha kwanza kwa kocha Thomas Tuchel.
  Katika mchezo huo ambao Chelsea ilimaliza pungufu kufuatia kutolewa kwa Thiago Silva kwa kadi nyekundu dakika ya 29 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano, mabao ya West Brom yamefungwa na Matheus Pereira dakika ya 45+2 na 45+4,  Callum Robinson dakika ya 63 na 90 na ushei na Mbaye Diagne dakika ya 68, wakati ya The Blues yamefungwa na Christian Pulisic dakika ya 27 na Mason Mount dakika ya 71
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WEST BROM YAICHAPA CHELSEA 5-2 PALE PALE DARAJANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top