• HABARI MPYA

  Friday, April 23, 2021

  KOCHA WA RAJA CASABLANCA ATUA YANGA SC KUKAMILISHA BENCHI LA UFUNDI LA WAARABU WATUPU

  ALIYEWAHI kuwa kocha wa mazoezi ya utimamu wa mwili wa Raja Club Athletic ya Morocco, Jawad Sabri amejiunga na vigogo wa soka nchini, Yanga SC.
  Sabri, raia wa Morocco aliyesoma na kufanya kazi Ufaransa ametambulishwa jana na uongozi wa Yanga SC, siku moja tu baada ya klabu hiyo kutangaza kuingia makubaliano ya ushirikiano na Raja Casablanca.
  Sasa benchi la Ufundi la Yanga linakamilishwa na wataalamu kutoka Kaskazini mwa Afrika watupu, chini ya Kocha Mkuu, Mohamed Nasreddine Nabi na Msaidizi wake, Sghir Hammadi wote wa Watunisia waliosaini mikataba ya mwaka mmoja na nusu kila mmoja juzi.


  Hatua hiyo inakuja baada ya Yanga SC kuachana na Mrundi, Cedric Kaze aliyefukuzwa mwezi uliopita baada ya kujiunga na timu Oktoba mwaka jana kufuatia kufukuzwa kwa Mserbia, Zlatco Krampotic aliyeanza na timu mwanzoni mwa msimu, Agosti mwaka jana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOCHA WA RAJA CASABLANCA ATUA YANGA SC KUKAMILISHA BENCHI LA UFUNDI LA WAARABU WATUPU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top