• HABARI MPYA

  Sunday, April 25, 2021

  SIMCHIMBA AIFUNGIA MABAO MAWILI IHEFU SC YAICHAPA COASTAL UNION 3-0 UWANJA WA HIGHLAND ESTATE


  TIMU ya Ihefu SC imeichapa Coastal Union ya Tanga mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Highland Estate, Ubaruku, Mbarali mkoani Mbeya.
  Mabao ya Ihefu SC yamefungwa na Andrew Simchimba mawili dakika ya 20 na 33 na Raphael Daudi dakika ya 36 na kwa ushindi huo timu hiyo iliyopanda Ligi Kuu msimu huu inafikisha pointi 30 baada ya kucheza mechi 28 na kupanda nafasi ya 13.
  Coastal Union yenyewe inabaki na pointi zake 33 za mechi 28 sasa katika nafasi ya 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMCHIMBA AIFUNGIA MABAO MAWILI IHEFU SC YAICHAPA COASTAL UNION 3-0 UWANJA WA HIGHLAND ESTATE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top