• HABARI MPYA

  Wednesday, April 21, 2021

  NAMUNGO FC YAENDELEA KUBORONGA MICHUANO YA AFRIKA, NA LEO IMECHAPWA 3-0 NA RAJA DAR

   

  TIMU ya Namungo FC leo imechapwa mabao 3-0 na Raja Club Athletic ya Morocco katika mchezo wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Raja yamefungwa na 
  Ilias Haddad dakika ya nane, Fabrice Ngoma dakika ya 14 na Zakaria Habti dakika ya 36.
  Kwa matokeo hayo, Namungo kutoka Ruangwa mkoani Lindi imefikisha mechi tano za kundi hilo bila kuvuna hata pointi moja ikifungwa nyumbani na Raja na Nkana FC ya Zambia, huku mechi nyingine ikifungwa nyumbani na Pyramids ya Misri.
  Namungo itasafiri kuwafuata Pyramids Jijini Cairo kwa mchezo wa mwisho Aprili 28.
  Leo Pyramids imeichapa Nkana FC 1-0, bao pekee la Abdalla El Said dakika ya 78 Uwanja wa Levy Mwanawasa Jijini Ndola, Zambia.
  Raja inaendelea kuongoza kundi hilo kwa pointi zake 15 sasa, ikifuatiwa na Pyramids pointi tisa na Nkana FC pointi sita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAMUNGO FC YAENDELEA KUBORONGA MICHUANO YA AFRIKA, NA LEO IMECHAPWA 3-0 NA RAJA DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top