• HABARI MPYA

  Wednesday, April 07, 2021

  VINICIUS APIGA MBILI REAL MADRID YAICHAPA LIVERPOOL 3-1


  TIMU ya Real Madrid imeutumia vyema Uwanja wa nyumbani, Alfredo Di Stéfano Jijini Madrid baada ya kuichapa Liverpool mabao 3-1 katia mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa usiku wa Jumanne.
  Mabao ya Real Madrid ya kocha Mfaransa, Zinedine Zidane yamefungwa na Vinícius Júnior mawili dakika ya 27 na 65 na Marco Asensio dakika ya 36, wakati la Liverpool ya kocha Mjerumani, Jurgen Klopp limefungwa Mmisri, Mohamed Salah dakika ya 51.
  Timu hizo zitarudiana Aprili 14 Uwanja wa Anfield Liverpool wakitakiwa kushinda 2-0 kwenda Nusu Fainali.
  x

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: VINICIUS APIGA MBILI REAL MADRID YAICHAPA LIVERPOOL 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top