• HABARI MPYA

  Wednesday, April 21, 2021

  RUVU SHOOTING YAFANYA MAUWAJI MABATINI, YAITANDIKA MWADUI FC 5-1 MLANDIZI

   

  TIMU ya Ruvu Shooting leo imeiadhibu Mwadui FC kwa kuichapa mabao 5-1 katika mchezo wa Ligo Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
  Mabao ya Ruvu inayofundishwa na kocha Charles Boniface Mkwasa yamefungwa na Edward Charles Manyama dakika ya 17, Shaaban Msala dakika ya 37 na 82, David Richard dakika ya 48 na Abrahman Mussa dakika ya 76, wakati la Mwadui limefungwa na Mohamed Hashim dakika ya 57.
  Ruvu Shooting inafikisha pointi 37 baada ya kucheza mechi 26, wakati Mwadui hali ni mbaya ikibaki na pointi zake 16 za mechi 37 mkiani mwa ligi ya timu 18.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, bao pekee la Kibu Dennis dakika ya 52 limeipa Mbeya City ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Polisi Tanzania Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
  x
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RUVU SHOOTING YAFANYA MAUWAJI MABATINI, YAITANDIKA MWADUI FC 5-1 MLANDIZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top