• HABARI MPYA

  Sunday, April 18, 2021

  BOCCO AFUNGA BAO PEKEE KIPINDI CHA PILI SIMBA SC YAWACHAPA MWADUI FC 1-0 KAMBARAGE

   

  BAO pekee la Nahodha John Raphael Bocco leo limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mwadui FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
  Bocco amefunga bao hilo dakika ya 66 kwa kichwa akimalizia mpira uliounganishwa kwa kichwa pia na beki Mkenya, Joash Onyango kufuatia kona ya winga Mghana, Bernard Morrison kutoka upande wa kulia.
  Ushindi huo unawafanya Wekundu hao wa Msimbazi wafikishe pointi 52 baada ya kucheza mechi 22 na kurejea nafasi ya pili, sasa wakizidiwa pointi mbili na Yanga SC ambao hata hivyo wamecheza mechi tatu zaidi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BOCCO AFUNGA BAO PEKEE KIPINDI CHA PILI SIMBA SC YAWACHAPA MWADUI FC 1-0 KAMBARAGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top