• HABARI MPYA

  Monday, April 05, 2021

  SAMATTA AFUNGA BAO PEKEE FENERBAHCE YASHINDA 1-0 KATIKA LIGI KUU YA UTURUKI


  BAO pekee la Mbwana Ally Samatta leo limeipa 
  Fenerbahçe ushindi wa 1-0 dhidi ya Denizlispor katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uturuki Uwanja wa Ülker Fenerbahçe Şükrü Saracoğlu Spor Complex Jijini İstanbul.
  Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Tanzania mwenye umri wa miaka 28, alifunga bao hilo dakika ya 64 akimalizia pasi ya beki Mturuki, Caner Erkin. 
  Kwa ushindi huo, Fenerbahçe inafikisha pointi 62 baada ya kucheza mechi 31 na kupanda nafasi ya pili ikizidiwa pointi mbili na Beşiktaş inayoongoza na mechi moja mkononi, wakati Denizlispor inayobaki na pointi zake 25 baada ya kucheza mechi 30 inaendelea kushika mkia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AFUNGA BAO PEKEE FENERBAHCE YASHINDA 1-0 KATIKA LIGI KUU YA UTURUKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top