• HABARI MPYA

  Friday, April 30, 2021

  YANGA SC YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA TFF BAADA YA KUICHAPA TANZANIA PRISONS 1-0 SUMBAWANGA BAO LA YACOUBA SOGNE

  VIGOGO, Yanga SC wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji Mburkinabe Yacouba Sogne dakika ya 54 akimalizia pasi ya kiungo Mrundi, Said Ntibanzokiza.
  Yanga inaungana na Rhino Rangers ya Tabora, Biashara United ya Mara, Mwadui FC ya Shinyanga na Azam FC ya Dar es Salaam pia kuwa timu zilizotinga Nane Bora hadi sasa.
  Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi kati ya Dodoma Jiji FC na KMC Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na Simba SC na Kagera Sugar Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam wakati keshokutwa JKT Tanzania watamenyana na Namungo FC Uwanja wa Jamhuri, Dodoma kukamilisha Hatua ya 16 Bora.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA TFF BAADA YA KUICHAPA TANZANIA PRISONS 1-0 SUMBAWANGA BAO LA YACOUBA SOGNE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top